Kujua haki zangu
HAKI NA WAJIBU WA MTUMIAJI
Haki ya kusafiri Salama
Mtumiaji ana haki ya kusafirisha bidhaa na kusafiri salama bila kuhatarisha afya na maisha yake.
Haki ya kuchagua
Mtumiaji ana haki ya kuchagua bidhaa au huduma bora kwa bei nafuu bila njia zozote zile za ulaghai au udanganyifu.
Haki ya kupata habari
Mtumiaji ana haki ya kupata habari sahihi na kamili kuhusu huduma au bidhaa anayotarajiwa kuuziwa.
Haki ya kupata fidia
Mtumiaji anahaki ya kupata fidia inayostahili kwa madhara yanayotokana na bidhaa au huduma isiyoridhisha.
Haki ya kupata huduma muhimu
Mtumiaji anahaki ya kupata huduma kwa maana ya haki ya bidhaa na huduma muhimu kwa maisha ya kila siku.
Haki ya kusikilizwa
Mtumiaji anahaki ya kutoa mawazo kwa mambo yanayogusa maslahi ya watumiaji katika soko na kuwakilishwa ipasavyo.
Haki ya kupewa Elimu
Mtumiaji anahaki ya kupata Elimu stahili ili kuelewa mambo yote ya msingi katika soko.
Haki ya kuishi katika mazingira mazuri
Mtumiaji anahaki ya mazingira salama yanayoweza kuhatarishwa na wafanyabiashara katika soko.
Shime zingatia Haki hizi nane na tusimame imara katika soko!