emblem

The United Republic of Tanzania

Tanzania Civil Aviation Authority-Consumer Consultative Council (TCAA-CCC)

News

TANGAZO LA MNADA WA HADHARA


Wananchi wote mnatangaziwa kwamba Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Anga (TCAA CCC) litauza kwa njia ya mnada wa hadhara mali chakavu siku ya Jumamosi, tarehe 14 Januari, 2023 kuanzia saa tatu asubuhi katika Ofisi za Baraza zinazopatikana Kinondoni karibu kabisa na Ubalozi wa Ufaransa. Mali hizi chakavu zinajumuisha vifaa vya tehama , vifaa vya Ofisi na samani za Ofisi.

MASHARTI YA MNADA

• Chombo/Kifaa kitauzwa kama kilivyo na mahali kilipo.

• Atakayetaja bei ya juu kabla ya nyundo kugongwa ndiye atakayeuziwa kifaa.

• Aliyetaja bei ya juu siyo lazima auziwe kama bei hiyo haijafikia bei elekezi.

• Kwa vifaa na samani,Mnunuzi atatakiwa kulipa papohapo asilimia mia moja (100%) ya thamani ya chombo/kifaa alichonunua.Mnunuzi akishindwa kutimiza sharti hili atakosa haki zote za ununuzi wa chombo/kifaa husika.

• Mnunuzi ataruhusiwa kuchukua vifaa vyake kutoka eneo la Baraza lililotajwa hapo juu baada ya kukamilisha malipo yote.

LIMETOLEWA NA:

KATIBU MTENDAJI,

BARAZA LA USHAURI LA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA USAFIRI WA ANGA ,

JENGO LA WAKALA WA MAJENGO TANZANIA (TBA),

MAKUTANO YA BARABARA YA ALI HASSAN MWINYI NA KILIMANI,

S.L.P 12242, DAR ES SALAAM.

Kwa Maelezo zaidi piga simu 0742 427747